Skip to main content

[RwandaLibre] CHADEMA yaonya Tanzania kutumiwa na waasi wa FLDR

 

 

CHADEMA yaonya Tanzania kutumiwa na waasi wa FLDR

Wenje onya Tanzania kutumiwa na waasi wa FLDR
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa msimamo wake kuhusu mahusiano yanayolegalega kati ya Tanzania na Rwanda, huku kikitaka ukweli ujulikane na suluhu itafutwe ili nchi hizo jirani zisiingie katika vita.
 
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana, Hezekia Wenje, aliwaambia waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam kuwa kuna ripoti zilizonukuliwa na gazeti la serikali ya Rwanda (News of Rwanda) kuwa waasi wawili wa Chama cha Rwanda National Congress (RNC), Dk. Theogene Rudasingwa na Condo Gervais pamoja na makamanda wa ngazi ya juu wa kikundi cha waasi wa FDLR walifanya kikao kilichoitwa cha malengo mahusi jijini Dar es Salaam.
 
Wenje aliongeza kuwa mratibu wa chama hicho, Condo Gervais pamoja na Rutasingwa waliwakilisha chama cha RNC huku Mtendaji Mkuu, Luteni Kanali Wilson Irategeka na Kanali Hamadi wakiwakilisha FLDR.
 
"Wiki moja kabla ya ripoti hiyo, gazeti la serikali ya Rwanda  liliandika kuwa waziri mkuu wa zamani wa Rwanda, Faustini Twagiramungu, alikuwa nchini tangu Januari 19, 2014 kabla ya kusafiri kuelekea Lyon nchini Ufaransa ambako alitoa taarifa ya kikao cha Dar es Salaam mbele ya mkutano wa wajumbe wa chama chake na kupongezwa baada ya kusema sasa wapo tayari kuing'oa Serikali ya Rwanda hata kwa bunduki," alisema Wenje.
 
Wenje alisema kuwa gazeti hilo la Rwanda lilieleza pia kuwa Desemba 20 mwaka 2013, Luteni Kanali Wilson Irategeka na Kanali Hamadi walisafiri toka Tanzania kwenda Msumbiji kwa kutumia hati za kusafiria za Tanzania kwa mazungumzo na watu wanaodaiwa kuwa ni mamluki wa chama cha RNC.
 
Kutokana na taarifa hizo, CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini, kimeitaka serikali kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo, hasa zile za pasi za kusafiria na kujiridhisha kuwa jina la Tanzania halitumiki vibaya kwa kuhusishwa kuwafadhili watu ambao wanataka kuiondoa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Rwanda.
Pili, CHADEMA imelitaka Bunge kupitia Kamati ya Mambo ya Nje inayoongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kuunda kamati ndogo ili ifuatilie tatizo lililopo kati ya Rwanda na Tanzania ili ukweli ujulikane na  mgogoro huo utafutiwe suluhisho mapema kuepusha vita inayoweza kutokea kwa nchi hizi jirani ambazo zote zipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Wenje aliongeza kuwa CHADEMA inataka kujua iwapo kama kuna maofisa wa juu wa Serikali ya Tanzania ambao kwa maelekezo au kwa sababu zao binafsi walishiriki katika utoaji wa hati za kusafiria kwa raia ambao si Watanzania kwani ni kosa kubwa katika mikataba ya kidiplomasia.
 
Tatu, CHADEMA kimeitaka serikali imwonye Twagiramungu ili abainishe kama alikuja Tanzania kufanya nini, na aeleze nia yake ya kusema kuwa alikuwa katika kikao mahususi hapa nchini, jambo ambalo limesababisha kusuasua kwa mahusiano ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo, CHADEMA kimesema serikali imtake Twagiramungu afute kauli yake, aombe radhi Watanzania kwa kuharibu mahusiano ya Tanzania na Rwanda, na kuharibu sifa ya Tanzania kuonekana inafadhili waasi, jambo ambalo ni kinyume kabisa na mkataba wa Afrika.
 

__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)
=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=--=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-
.To post a message: RwandaLibre@yahoogroups.com; .To join: RwandaLibre-subscribe@yahoogroups.com; .To unsubscribe from this group,send an email to:
RwandaLibre-unsubscribe@yahoogroups.com
_____________________________________________________

More news:  http://amakurunamateka.blogspot.co.uk/; http://ikangurambaga.blogspot.co.uk/
--------------------------------------------------------------------------
.

__,_._,___

Comments

Popular posts from this blog

[AFRICAFORUM] Tr : [hinterland1] Tr : L'OCCUPATION RWANDAISE EN MARCHE

  ----- Mail transféré ----- De : Mpania Jean <drjeanmpania@yahoo.fr> À : Hinterland <hinterland1@yahoogroupes.fr> Envoyé le : Mercredi 26 février 2014 17h13 Objet : [hinterland1] Tr : L'OCCUPATION RWANDAISE EN MARCHE   Le Mercredi 26 février 2014 9h56, congokdp <congokdp@gmail.com> a écrit : L'OCCUPATION RWANDAISE EN MARCHE :   Voici comment les institutions et tout le système de sécurité de la RDC sont sous contrôle du Rwanda et les officiels congolais infiltrés par des «hirondelles» rwandaises! L'OCCUPATION RWANDAISE EN MARCHE :  Voici comment les institutions et tout le système de sécurité de la RDC sont sous contrôle du Rwanda et les officiels congolais infiltrés par des «hirondelles» rwandaises! Le processus d'occupation de la RDC par le lobby tutsi rwandais passe par le...

[haguruka.com] Fw: *DHR* New Vision, Uganda @Gen Fred Rwigyema's untold story.

  On Sunday, 22 November 2015, 18:52, "Jean Bosco Sibomana sibomanaxyz999@gmail.com [Democracy_Human_Rights]" <Democracy_Human_Rights@yahoogroupes.fr> wrote:   Gen Fred Rwigyemas untold story By Muwonge Magembe The death of Gen. Aronda Nyakairima on September 12; eclipsed the 25th year death memorial of Maj. Gen. Fred Rwigyema which is commemorated every October. Rwigyema died strangely in October, 1990, after launching a military invasion against President Juvenal Habyarimana. Before he left for Rwanda, Rwigyema parked a coffee brown Mercedes Benz (G-Class) near the residence of then special administrator for Mbarara district, Henry Rwigyemera. Rwigyema started living in Uganda when he was only three years following his parents' relocation from Mukiranze village, Kamonyi district, Rwanda to Nshungerezi refuge camp, Ankole and Kahungye, Toro. Their relocation was motiv...

Fw: [ibukabose_rengerabose] Fw: Rwanda: deteriorating human rights and security situation

 Rwanda: deteriorating human rights and security situation   r w an d ab ri d ge b u il d er s@ gmail.c om H.E. Amb. Smail Chergui, Commissioner, Peace and Security, African Union (AU) Addis Ababa, Ethiopia October 20, 2020 Your Excellency, We, a coalition of 37 organizations, write to you in your capacity as the Ch airperson of the African Commission on Peace and Security (The Commission), to appeal you to urgently address the deteriorating human rights and security situation in Rwanda. We reiterate that Rwanda continues to face allegations of human rights violations that are of an extremely serious nature. These allegations have been found credible by none less than Human Rights Watch, Amnesty International and UN panel on human rights. Several well-grounded allegations exist about the extreme lack of fundamental freedoms in Rwanda, which it is charged, has resulted in serio us violation...